Katika Khutba yake, Sheikh Suleiman alieleza nafasi muhimu ya maadili katika ujumbe wa vyuo vya dini na jukumu la wanazuoni katika kulea jamii yenye maadili mema kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - Kikao cha kielimu na maarifa (Taaluma) kimefanyika leo hii Tarehe 19 Julai, 2025 -
Katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s.a.w.w) - Dar-es-salaam, kikiwa na mada hii: “Nafasi ya Vyuo vya Dini katika Kukuza Maadili ya Kijamii”.
Washiriki katika Kikao hiki ni Wanafunzi wa Kidini wa Chuo hiki.
Muwasilishaji wa Mada: Hujjatul Islam wal-Muslimin Sheikh Suleiman Issa.
Katika Khutba yake, Sheikh Suleiman alieleza nafasi muhimu ya maadili katika ujumbe wa vyuo vya dini na jukumu la wanazuoni katika kulea jamii yenye maadili mema kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Alisisitiza kuwa vyuo vya dini vina wajibu mkubwa wa kueneza utamaduni wa kuwajibika, kuheshimiana na kuhudumia jamii.
Kikao hiki, kilihitimishwa kwa maswali na majibu, huku washiriki wakionyesha hamasa ya kujadili masuala ya kijamii na kimaadili kwa kina zaidi.
Your Comment